Wednesday, May 28, 2014

ASILIMIA 50 ya vijana hawana maarifa ya kutosha juu ya masuala ya afya ya uzazi



WADAU   wa Maendeleo wakiwemo UNESCO, WHO, UN AIDS, UN,SIDA  wameahidi  kutoa  ya Dola za Marekani 450,000 kwa ajili ya utekelezaji wa mpango kazi wa maazimio ya wakuu wa  nchi 20 , juu ya utoaji wa Elimu ya Afya ya Uzazi na maadili kwa vijana waliopo katika shule za msingi na sekondari kwa lengo la kuwawezesha wanafunzi kuepuka  mimba za utotoni na kujikinga na maambukizi ya virusi vya ukimwi.



Akizungumza katika mkutano huo jijini Dar es salaam, Afisa wa Elimu ya Ukimwi na Afya kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO  bwana Mathias Herman amesema katika utekelezaji wa maazimio hayo, Tanzania inatarajiwa hadi kufikia mwaka 2015 kutekeleza maudhui ya utoaji wa Elimu ya Afya ya Uzazi kwa wanafunzi wa shule hizo


Amesema Takwimu za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi zinaonyesha kuwa , Takriban wanafunzi 6,000 kutoka katika shule za msingi na sekondari hapa nchini wanaacha masomo kutokana na mimba za utotoni, kutokana na kukosa elimu ya masuala hayo, ambapo kati ya hao asilimia 40 wanatoka katika shule za msingi na asilimia 60 wanatoka katika shule za sekondari.

Amesema imebainika kuwa asilimia 50 ya vijana  hawana maarifa ya kutosha  juu ya masuala ya afya ya uzazi, hali inayosababisha  vijana hao kuanza mahusiano ya kingono wakiwa na umri chini ya miaka 15



No comments:

Post a Comment