SHIRIKA la kuhifadhi misitu ya asili Tanazani TFCG kupitia mradi wa kuongeza thamani katika misitu AVA limeanza kuhamasisha jamii zinazoishi kando ya misitu kujiunga katika vikundi vya hisa kujipatia kipato na kuepuka uharibifu wa mazingira.
Hayo yameelezwa na
Meneja wa Mradi wa AVA Bwana Hassan Chikira kwenye mapitio ya mradi
unatekelezwa katika vijiji 31 wilayani Mvomero mkoa Morogoro.
Kwa mujibu wa Chikira
vikundi hivyo kupitia mradi wa AVA vitawarahisishia kupata fedha za kuendesha
miradi mingine na kuachana mpango wa kutumia maliasili misitu kama itega uchumi
vyao katika maisha.
Mwenyekiti wa kikundi
Benedict matei na Mwalimu wa kikundi cha hisa Shaban Mganga walisema kupitia
vikundi hivyo wanakikundi sasa wanakoposheka na kuanzisha biashara na sghuguli
ndogo ndogo za kuwaingizia kipato.
Mradi wa AVA umelenga
kuhakikisha jamii inayozunguka misitu inaacha tabia ya kutumia misitu kama
chanzo cha kipato chao na badala yake kufanya shughuli nyingine na
wanahifadhi misitu.
No comments:
Post a Comment