MKAGUZI
mkuu wa shule wilayani kilosa Ally Abdulhaman
amewataka wadau wa elimu kufuata kanuni na taratibu za kuanzisha shule pamoja
na vyuo.
Ameyasema hayo ofisini kwake wakati
akizungumzia usajili wa Snai Media school iliyopo manzese wilayani kilosa na
kusema kuwa shule hiyo haikusajiliwa tangu ilipoanzishwa mwaka 2009 na kusema
kuwa walishatoa maelekezo kwa mmiliki wa shule hiyo kuwa ataje usajili wa shule
hiyo mapema na kuongeza kuwa shule hiyo iliamuliwa kufungwa na mkaguzi wa mkoa
mnamo tar 31 january lakini shule hiyo bado inaendelea kutoa mafunzo hayo ya
elimu.
Aidha amesema kuwa wahisani hao
huanzisha shule hizo kwa kupitia ofisi ya ustawi wa jamii yaani child care
lakini ndani yake hutoa elimu ambapo ni kinyume na taratibu na sheria na
kubainisha kuwa watoto kuanzia umri wa miaka 0 hadi 4 ndio wanaotakiwa kuwa
kwenye child care na wanapofikia umri wa miaka 5 huyo anakuwa na umri wa kuanza
elimu ya awali.
Naye mkurugenzi wa Snai media school
Mery Paul Komba amesema kuwa shule yake ipo kwenye mchakato wa kuisajili likini
pia amesema kuwashule hiyo bado ipo chini ya ustawi wa jamii na wapo kwenye
mpango wa kuisajili lakini serikali inawapelekesha haraka na wanashindwa cha
kufanya kwa sababu wanachanganywa na kuongeza kuwa swala la kufungwa kwa shule
hiyo limewaumiza sana wazazi wenye watoto katika shule hiyo na kueleza kuwa
elimu wanayoipata watoto katika shule hiyo ni nzuri na wanaumizwa wanapooona
shule hiyo inataka kufungwa.
Aidha ameongeza kwa kusema kuwa
lengo la kuanzisha shule hiyo ni kutokana na kuona kiwango cha elimu kinashuka
na changamoto kubwa na swala la lugha ya kiingereza.
Nao wanafunzi katika shule hiyo ya
Snai media school shurut palma na careen fredy wamesema kuwa changamoto
inayowakabili shuleni hapo ni kutokuwepo maji kalibu pia vyoo kutofanyiwa usafi
ulio sahihi kwa usalama wa
No comments:
Post a Comment