Wednesday, May 21, 2014

MKUU wa wilaya asitisha shughuli za uzalishaji wa madini wilayani Mvomero.


MKUU wa wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro bwana Antony Mtaka amesitisha  shughuli  za uzalishaji na ujenzi wa  wa kiwanda cha madini katika kijiji cha Melela Mlandizi baada ya mwekezaji kubainika kutofuata taratibu za kisheria.

Bwana Mtaka ametoa kauli hiyo wakati wa mkutano wa viongozi na wanakijiji ambao wameulalamikia uongozi wa kijiji hicho kufanya mikataba pasipo kuwashirikisha wananchi.

Amesema uongozi wa wilaya umebaini kuwa mwekezaji amepewa ardhi kinyume cha taratibu ambapo maombi yaliishia kwenye halmashauri ya kijiji  pasipo kuthibitishwa na idara za madini,ardhi,mazingira na ridhaa ya wanakijiji.

.
Hata hivyo amemtaka mwekezaji huyo kufika ofisi ya mkurugenzi mtenda wa halmashauri ya wilaya ya Mvomero ili kupata barua yenye nukuu za kisheria kutoka wizara ya madini ili imsaidie kupata uhalali wa kupata leseni, ridhaa ya wanakijiji na kumwezesha  kufanya shughuli zake kihalali.



No comments:

Post a Comment