Wednesday, May 21, 2014

WAKULIMA nchini watakiwa kushirikiano na wataalamu wa kilimo ili waweze kunufaika na utaalamu wao



 

WAKULIMA  nchini wametakiwa kuwa karibu na wataalamu wa Kilimo ambao watawasaidia katika masuala mbalimbali ya kilimo yatakayoweza kuwanufaisha ili kuepukana na kilimo kisichokuwa na tija.

Ushauri huo   umetolewa jana na Meneja Masoko wa kampuni ya uzalishaji mbegu za nafaka SEEDCO,bwana Sillas Ngowe wakati wa maadhimisho ya siku ya wakulima iliyofanyika katika kijiji cha Vikenge kilichopo Kata ya Mzumbe wilayani Mvomero mkoani Morogoro.

Siku ya wakulima katika kijiji cha Vikenge wilayani Mvomero mkoani Morogoro imeandaliwa na kampuni ya uzalishaji mbegu za nafaka ya Seed Co kwa kushirikiana na kampuni za Bayer,Opportunity,Syngenta pamoja na wakala wa usambazaji pembejeo za Kilimo mkoani Morogoro Imuka Agricultural Enterprises.

No comments:

Post a Comment