SHEHENA yenye zaidi ya tani 24,000 za Sukari imedoda katika
maghara ya Kiwanda cha Sukari ILLOVO Kilombero na kuhatarisha ajira za
wafanyakazi kiwandani hapo samnbamba na kukua kwa umasikini wilayani
Kilombero.
Kudoda kwa shehena hiyo kunkwenda
sambamba na lawama dhiidi ya serikali kudawiwa kuruhusu kwa holele kuingizwa
kwa Sukari nyingi kutoka nje ya nchi inyouzwa kwa bei nafuu tofauti na
inayozalishwa nchini.
Mbele ya Naibu waziri wa Kilimo,chakula
na Ushirika Godfrey Zambi, Kaimu mkurugenzi mkuu wa kiwanda cha Ilovo Joseph
Rugaimukamu na Mwakilishi wa Bodi ya Sukari nchini Abdul Mwankemwa
walisema mbali na hujuma hiyo wafanyabiashara wanatumia mifuko yenye nembo
ya viwanda vya nchini kujaza sukari ya nje.
Walisema hujuma
hiyo imesababisha viwanda kushindwa kulindwa kwa kuruhusu shehena za
bidhaa hiyo kuingizwa nchini hivyo makampuni ikiwemo
Illovo kushindwa kujiendesha na kuelemewa na mzigo wa madeni ya
wafanyakazi,wakulima na taasisi nyingine zikiwemo za kifedha.
"iwapo TRA
hawatadhibiti hali hii kuna hatari viwanda vingi vikajifunga kwa kushindwa
kujiendesha baada ya bidhaa zake kukosa soko"alifafanua Rugaimukamu.
No comments:
Post a Comment