SHIRIKA la world vision lililoanzishwa mwaka 1959
nchini Marekani na kuingia nchini Tanzania mwaka 1980 leny elengo la kuleta
ustawi wa mtoto kuwa na maisha mazuri, Afya njema na kumjua mungu , limetoa
mafunzo ya ujasiriamali kwa vikundi vya vikoba wilayani kilosa.
Katika mafunzo hayo yaliyohudhuriwa
na wajumbe kutoka katika vikundi mbalimbali katika kutoa mafunzo hayo
wamewezeshwa jinsi ya kuendesha vikundi vyao na taratibu na kanuni za kufuata
katika kuendesha vikundi vyao.
Naye meneja wa mradi wa Ulaya ADP
katika shirikala world vision Mathias Mwingila
amesema kuwa katika kutoa mafunzo hayo
wanakumbana nachangamoto mbalimbali
ikiwemo baadhi ya wanavikundi kudai posho wakati wanapoitwa kupewa mafunzo na
kusema kuwa lengo la world vision n ikutoa mafunzo ya kuweza kujikwamua kimaisha
na kuleta maendeleo katika jamii.
Aidha ameongeza kuwa changamoto
nyingine ni mapokeo hasi kwa baadhi ya wajumbe wakidhani kuwa world vision
inaeneza dini ya kikristo kutokana na shirika hilo kuanzishwa na watu wa dini
ya kikristo na amebainisha kuwa shirika hilo halipo upande wowote wakidini ila
lipo kwaajili ya kutoa mafunzo ya kujikwamua kimaisha kwa wajasiriamali
wadogowadogo.
No comments:
Post a Comment