CHUO cha mafunzo ya jinsia nchini GTI ikishirikiana na asasi ya
DELOITTE kupitia mradi wa TUNAJALI II wamebaini kuwa vyanzo vya umasikini
nchini vinasababbishwa na ongezeko la ukatili na bajeti kutozingatia jinsia.
Hayo yamebainishwa na Mratibu wa
mafunzo ya ushawishi na utezi kutoka GTI Donard Donard yenye lengo la
kuleta usawa wa kijinsia katika masuala ya VVU Ukimwi ,haki za binadamu na
Matumizi ya fedha za umma kwa asasi za kijamii mjini hapa.
Linguine lililojitokeza ni pamoja na
walengwa kutoelewa mbinu za kushiriki katika mchakato na kufuatilia bajeti
zinazowahusu,utengwaji rasilimali fedha kidogo katika mapambano dhii ya
VVU Ukimwi,mtazamo hasi juu ya shuguli za AZISE na uhaba wa wataalamu wa
kujengea uwezo watumishi seriaklini na kwenye AZISE.
Alisema washiriki baada ya mafunzo
watapata fulsa ya kupanga Bajeti zinazozingatia jinsia,kuelekeza shuguli za VVU
Ukimwi na Awaki kijinsia,kuendesha harakati za ushawishi na utetezi hasa
kijinsia na kushiriki katika ufuatiliji wa rasilimali fedha za umma pia kudai
uwajibikaji kwa viongozi.
No comments:
Post a Comment