Kamnda wa mkoa wa Morogoro(kulia) akiwa na mkuu wa mkoa Joel Bendera (kushoto) |
MWANAMKE mmoja Neema Sanga(33) mkazi wa Mngeta wilayani Kilombero ,mkoa
wa Morogoro ameuwawa nyumbani kwake kwa kuchalangwa na mapanga sehemu
mbalimbali za mwili na mtu naedaiwa kuwa mumewe Laurian Labani kwa wivu wa
mapenzi.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake,Kamanda wa Polisi mkoa hapa Leonard Paul alisema tukio hilo lilitokea septemba 25 saa 3 usiku baada ya kuhitilafiana na kunyimamna unyumba kwa muda mrefu.
Kamanda huyo aliongeza kabla ya kuuwawa Neema alikatwa na Panga hilo shigoni,taya la kulia na kwenye paja ambapo alipiga kelele na watu kukusanyika ambapo walifanikiwa kumpa msaada na alifariki kabla hajapata msaada.
Wakati huohuo jeshi hilo linawashikilia watu watatu akiwemo dereva Hassan Yasin,utingo Frenki John wenye gari Mitisubishi Fussona T 703 AUY na Rashid Ramadhani(45)'Duge'wa Doma Mvomero wakisafirisha Bangi kwenda jijini Dar es salaam.
Kamanda Paul alisema kukamatwa kwa
watuhumiwa hao kulitokana na asikari wa usalama barabarani kilishitukia lori
hilo na kulifanyia upekuzi ambapo baada ya upekuzi ilibainika kubeba samaki na
viroba vya bangi.
watuhumiwa wote bado wanashikiliwa
na jeshi la polisi kwa mahojiano zaidi na muda wowte kuanzia sasa watapandishwa
kizimbani kujibu makosa yanyowakabili.
No comments:
Post a Comment