SERIKALI nchini Tanzania imeombwa kupunguza kodi ya mazao ili
kuwawezesha wakulima kukabiliana na changamoto za kiuchumi zinazowakabili.
Hayo yamebainishwa hivi karibuni na Mwenyekiti
wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania,bwana Jarson Kalile wakati akiongea na wanahabari
jijini Dar es salaam.
Bwana Kalile amesema kodi zilizo mzigo kwa
wakulima ni pamoja na ushuru wa halmashauri ya wilaya asilimia tano ya bei ya mkulima,
ushuru wa utafiti asilimia 0.75 ya bei ya mnadani, mfuko wa maendeleo ya kahawa
uliaonzishwa na wadau asilimia 0.5 ya bei ya mkulima, ada ya leseni ya kuuza
kahawa nje zinazotozwa na Bodi ya Kahawa (TCB).
Aidha Mwenyekiti huyo amezitaja ada za maghala, leseni, leseni ya kiwanda cha
kukoboa kahawa, ada ya kibali cha kuuza kahawa nje kwa njia ya mauzo ya moja
kwa moja pasipo kupitia mnadani na kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwenye
vifaa mbalimbali vya kuhudumia kahawa yakiwamo magunia kuwa ni kikwazo cha
maendeleo ya mkulima .

No comments:
Post a Comment