![]() |
| Mbunge wa Malinyi Dk Haji Mponda |
Dk Mponda aliamua kumwaga vifaa hivyo baada ya kutoridhishwa na
hali yake kutokana na kuchakaa baada ya kujionea alipo alipokitembelea juzi.
Akizungumza na watumishi wa kituo hicho,Dk Mponda aliiomba
serikali itafute njia nyingine ya kukisaidia kituo hicho cha afya ikiwemo
kuondoa tatizo la upungufu wa watumishi na madawa wakati mchakato wa
kupandisha hadhi kutoka kituo cha afya kwenda hospitali ukisubiriwa.
Alisema kituo hicho kina changamoto nyingi na ni bahati
mbaya katika jimbo zima na wilaya ya Malinyi kituo kinachofanya kazi ni
kimoja tu na nyingine ni hospitali ya binafsi ya Lugala inayomilikiwa na kanisa
la kilutheri.
Kwa mujibu wa Mbunge huyo changamoto zinazokikabili kituo hicho ni
pamoja na upungufu wa dawa na watumishi wachache na kusema kuwa
anashindwa kuzitatua changamoto hizo tokana na sera kuweka mipaka hasa kituo
cha afya kuwa na ikama ya watumishi na mgao wake wa dawa.
Ameshangazwa na sera hiyo na kutolea mfano kuwa ndani ya
miezi mitatu kituo hicho kinapata mgao wa shilingi milioni 2 za madawa wakati
hospitali ya wilaya Mahenge inapata shilingi milioni 20 ya mgao huo ndani ya
miezi hiyo mitatu huku kituo hicho kinahudumia wagonjwa wengi kuliko hospitali
ya wilaya.
Ametolea mfano kuwa kila mwezi kituo hicho kinapokea akinamama 150
wanaokuja kujifungua wakati hospitali ya wilaya hupokea akinamama 100 tu hivyo
kuiomba serikali kusaidia wilaya hiyo
kuwa mpya.

No comments:
Post a Comment