MKURUGENZI na mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Morogoro wapokelewa kwa mabango toka kata mpya ya Kibuko, makao makuu ya Halmashauri ya wilaya hiyo, Mvuha Morogoro vijijini .
Baadhi ya kero zilizoinishwa baada ya kuibuliwa na wanachi katani
humo kwa ushirikiano na Mtandao wa jinsia nchini TGNP ni pamoja na kata hiyo
kutelekezwa bila huduma za kijamii zikiwemo shule,kituo cha afya,maji safi na
salama,maafa yatokanayo na migogoro ya wakulima na wafugaji.
Katika risala yao iliyosomwa na Latifa Hussen mbele ya
kaimu mkurugenzi Ernest Khisombi na kaimu mwenyekiti wa halmashauri hiyo
Emilly Kidevu wanachi hao walisema mbali na kusongwa na changamoto hapo juu
kunajipu la uwekezaji uchwara wasio na manufaa nao bdalayake unawasababishia
maafa na maumivu kutokana na milipuko ya baruti zitumikazo mgodini
hapo.
“hizi ni baadhi ya kero zinazotukera kwa muda mrefu na kuja kwetu
hapa ni kupata majibu ya hatima yake nini na sisi tutanufaikaje na changamoto
hizo ikiwemo ya kutokuwa na huduma hata moja za kijamii sambamba na mgodi
uliopo Mwalazi unamanufaa gani kwetu…tunaomba majibu “alisema Latifa.
Alisema kata hiyo mpya kutoka kata mama ya Mkuyuni imetelekezwa
baada ya kujigawa na kuwaachia nawanchi mzigo mkubwausio na msaada kwao hasa
juu ya ujenzi wa miundombinu ya huduma za kijamii na kutokuwepo kwa faida ya
uwekezaji katika mgodi huo wa madini.

No comments:
Post a Comment