Shein ambaye aliapishwa leo baada ya kushinda uchaguzi wa
marudio uliosusiwa na upinzani amesema kuwa atafanya kila awezalo kuzima
majaribio yeyote ya kuitumbukiza kisiwa hicho katika uhasama.
Shein alitangazwa mshindi wa asili mia 90% ya kura zote
zilizopigwa Jumapili iliyopita.
Uchaguzi huo wa marudio uliitishwa baada ya kura iliyopigwa
mwezi Oktoba mwaka uliopita kufutiliwa mbali baada ya kiongozi wa upinzani
alidai kushinda.

No comments:
Post a Comment