![]() |
Makao makuu ya mamlaka ya hali ya hewa Duniani |
SHIRIKA hirika la Hali ya Hewa Duniani limetahadharisha wasiwasi wake kutokana na kuongezeka joto
katika sayari ya dunia,eneo la Pwani ya Afrika mashariki.
Katika kipindi cha siku
chache zilizopita, wataalamu wa hali ya hewa nchini Kenya na Tanzania wameonya
kuhusu kiwango cha joto kali katika miji ya Mombasa na Dar es Salaam na wakaazi
wa miji hiyo wametakiwa kuchukua hatua za kuzuia vifo vitokanavyo na joto kali.
Imetabiriwa kuwa miji hiyo inaweza kupata
kiwango cha joto la nyuzi 36 au zaidi katika siku chache zijazo.
Shirika la Hali ya Hewa
Duniani, WMO limesema kiwango cha joto kupindukia cha mwaka 2015 ni moja ya
viashiria hivyo.
WMO imedokeza viashiria
vingine kuwa ni mafuriko na ukame kupindukia, hali ya joto isiyotabirika,
kuongezeka kwa joto la maji ya bahari na kupungua kwa kiwango cha barafu.
WMO imesema tayari miezi
ya Januari na Februari mwaka huu imekuwa na viwango vya juu vya joto huku
barafu kwenye bahari ya Artic ikipungua na kuyeyuka kwa kasi isiyo ya kawaida.
Akifafanua zaidi kuhusu
hali inavyotabiriwa baadaye katika mazungumzo na waandishi wa habari huko
Geneva, Uswisi, Mkurugenzi mkuu wa WMO Petteri Taalas amesema katika karne
zijazo kiwango cha maji ya bahari kitaongezeka kwa mita moja zaidi kama joto
litaongezeka kwa nyuzi joto mbili.
Amesema iwapo hatua
hazitochukuliwa katika kupunguza hewa chafuzi basi tutashuhudia kiwango cha
maji ya bahari kikiongezeka kwa mita tano ifikapo mwaka 2500.
No comments:
Post a Comment