![]() |
Sadiq Hussein Jaberi Ansari |
Msemaji wa Wizara ya
Mambo ya Nje ya Iran amelaani shambulio la kigaidi lililofanywa katika msikiti
mmoja huko Nigeria.
Katika radiamali kwa
shambulio la kigaidi dhidi ya msikiti mmoja katika mji wa Maiduguri makao makuu
ya jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa Nigeria, Sadiq Hussein Jaberi Ansari,
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ametaka kuchukuliwa hatua za pande
zote ili kuendesha mapambano dhidi ya ugaidi.
Jaberi Ansari ametoa
mkono wa pole kwa familia za wahanga wa shambulio hilo la kigaidi huko Nigeria
na kueleza kuwa, kukaririwa jinai kama hiyo katika maeneo mbalimbali duniani,
kunaonyesha kuwepo udharura wa kuchukuliwa hatua za lazima ili kukabiliana
ipasavyo na kwa pande zote na ugaidi na suala la uchupaji mipaka.
Mlipuko uliotokea jana
katika msikiti mmoja huko Maiduguri makao makuu ya jimbo la Borno kaskazini
mashariki mwa Nigeria umeuwa watu 22 na kujeruhi wengine wengi; shambulio
ambalo kundi la Boko Haram limetangaza kuwa limehusika.
No comments:
Post a Comment