Thursday, March 17, 2016

WATAALAMU sita wa umoja wa Afrika kushuhudia uchaguzi Zanzibar

TUME  ya Umoja wa Afrika imetangaza kwamba itawatuma waangalizi wa uchaguzi wa marudio visiwani Zanzibar ambao utafanyika Jumapili.

Mwenyekiti wa tume hiyo Dkt Nkosazana Dlamini Zuma ameidhinishwa kutumwa kwa wataalamu sita wa kufuatilia uchaguzi huo wa tarehe 20 Machi.
Vyama sita vya upinzani, kikiwemo Chama cha Wananchi (CUF) vimetangaza kwamba vitasusia uchaguzi huo.
Uchaguzi huo unatokana na kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa urais na wawakilishi uliofanyika tarehe 25 Oktoba mwaka jana.
Chama cha CUF kilipinga hatua ya kufutwa kwa matokeo hayo.
Mgombea wake wa urais, Maalim Seif Sharif Hamad, alijitangaza mshindi wa uchaguzi huo wa mwaka jana.


No comments:

Post a Comment