Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kongo |
KAMANDA wa zamani katika Jeshi la
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amemtaka Rais Joseph Kabila wa nchi hiyo
kuondoka madarakani.
Elie Kapend Kanyimbu
jenerali wa zamani katika jeshi la DRC amesema Kabila anapaswa kuondoka
madarakani Novemba 19 mwaka huu baada ya kumalizika duru ya pili ya urais.
Jenerali huyo amepinga
pendekezo la Rais Kabila la kufanyika mazungumzo kuhusu uchaguzi ujao. Amesema
kile kinachotakiwa ni kufanyika kongamano huru la kitaifa. Kanyimbu ni
mwanzilishi wa kundi la wapiganaji wa AFDL ambalo lilimuondoa madarakani Mobutu
Seseseko mwaka 1997 kwa uungaji mkono wa Uganda. Hivi sasa Kanyimbu ni mkuu wa
chama cha upinzani cha FNLC.
No comments:
Post a Comment