Thursday, August 11, 2016

WAKULIMA wa korosho walia na ukosefu wa pembejeo

Wakulima wakiandaa miche ya korosho kwa kupanda shambani 
UKOSEFU wa pembejeo  za kilimo kwa zao la korosho kunachangia kwa kiasi kikubwa kwa zao hilo kuzalishwa chini ya kiwango imefahamika.

Hayo yamebainishwa hivi karibuni na wakulima wa zao hilo mkoani katika mahojiano na Mbiu Media wakati wakileleza sababu za kushuka kwa uzalishaji wa zao hilo.
Wakulima hao wamefafanua kuwa, bado uwekezaji wa kutosha wa kuwapatia elimu ya kuwajengea uwezo wakulima ipo chini hali inayochangia jitihada za wakulima kupungua .
 Imeelezwa kuwa katika msimu wa mwaka 2013/14, zao la korosho lilikuwa la pili kwa kuingiza fedha za kigeni nchini, huku zao la tumbaku likishika nafasi ya kwanza.


No comments:

Post a Comment