![]() |
| Waandamanaji nchini Brazil |
MAELFU ya wenyeji
wasio na makao mjini Sao Paolo waliandamana nje ya uwanja utakaoandaa mechi ya
kwanza ya kombe la dunia alhamisi ijayo wakipinga gharama ya juu ya mashindano
hayo.
Maandamano hayo
yaliwadia siku moja tu baada ya rais wa Brazil Dilma Rousseff kuwahakikishia
wageni na mashabiki wa kandanda kuwa kamwe hatoruhusu maandamano yatie doa
kwenye kipute hicho cha kombe la dunia.
Takriban waandamanaji
10,000 waliziba barabara zote mjini Sao Paolo wakiishinikiza serikali ya bi
Rousseff iwekeze katika sekta ya afya elimu na ipunguze gharama ya juu ya
usafiri wa umma.
Zaidi ya watu milioni
moja waliandamana katika barabara za miji yote ya Brazil wakishinikiza serikali
kupunguza ubadhirifu wa fedha na kupunguza matumizi yake kwa maandalizi ya
kombe la dunia na yale ya Olimpiki yatakayofanyika mjini Rio mwaka wa 2016.
Licha ya hakikisho la
rais Rousseff wafanyikazi wa reli walitishia kuanza mgomo upya huku polisi wa
trafiki mjini Sao Paolo pia wakitishia kuanza mgomo Alhamisi.

No comments:
Post a Comment