SERIKALI
imeingiza
jumla ya shilingi bilioni 6.8 kwa
kipindi cha mwaka 2013/3014 kutokana na kodi inayolipwa na mitandao ya simu nchini baada ya kuweka mtambo maalum wa kudhibiti udanganyifu
uliokuwa ukifanywa na wamiliki wa mitandao ya simu wasiokuwa waaminifu.
Waziri mawasiliano, sayansi na teknolojia
Profesa Makame Mbarawa amebainisha hayo mapema leo bungeni mjini Dodoma wakati
akiwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2014/2015.
Profesa Mbarawa amesema kuwa wizara kwa
kushiorikiana na tume ya mawasiliano nchini(TCRA) imeunda kamati maalum ya
ufuatiliaji ili kuendeleas kudhibiti na kuzuia hali hiyo isitokee sanajari na
kuongeza pato la Taifa kupitia mitandao ya simu.
No comments:
Post a Comment