Saturday, May 31, 2014

SERIKALI na wadau wa mazingira watakiwa kuandaa vipindi vingi vya elimu kwa umma kuhusu mazingira



WAKATI tukielekea katika maadhimisho ya siku ya mazingira duniani ,wananchi wa Mwanza wameitaka Serikali na wadau mazingira nchini kuandaa vipindi vya elimu kwa umma kupitia redio na luninga ili kukabiliana na changamoto zinazoikabili tasnia hiyo.

Wakiongea na waandishi wa habari leo asubuhi mjini Mwanza , baadhi ya wavuvi wa ziwa Victoria wamesema, bado elimu ya mazingira inahitaji kwa baadhi ya wavuvi kwani mapambanio ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi hayanabudi kuongezwa kasi.


Wamesema kuna baadhi ya wavuvi  wanashiriki katika vitendo vya uharibifu wa mazingira kutokana na  kutopata elimu ya kutosha kwani semina za mara moja kila baada ya miezi sita haikidhi mahitaji

Maadhimisho ya  siku ya mazingira duniani hapa nchini kitaifa yanafanyika jijini Mwanza  ambapo hufanyika kila tarehe 5, june  duniani kote.

Mkoa wa Mwanza umechaguliwa kutokana na changamoto za ukame unaoendelea katika mkoa huo na uharibifu mkubwa wa vyanzo vya maji kutokana na kilimo kisichoendelevu  na kutumia sumu na makokoro


No comments:

Post a Comment