Saturday, May 31, 2014

WANANCHI kijiji cha Usakazi , wilayani Bagamoyo waiomba wizara ya ardhi kuingilia kati ugawaji wa ardhi yaombvwa



SERIKALI kupitia Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeombwa kuingilia kati ugawaji wa ardhi unaofanywa na viongozi wa kijiji cha Visakazi kilichopo kata ya Ubena wilayani Bagamoyo mkoani Pwani kabla madhara hayajatokea.

Wakazi wa kijiji hicho wametoa ombi hilo jana wakati wakizungumza na Mbiu ya maendeleo ilipotembelea kijijini hapo kwa ajili ya kuzungumza na viongozi pamoja na wananchi juu ya zoezi hilo la ugawaji wa ardhi ambalo limekuwa likilalamikiwa na wananchi hao.

Wanakijiji hao akiwemo bwana Athuman Mgama na Samuel Anatory wamewatupia lawama viongozi wa kijiji kwa madai kwamba wamekuwa wakigawa ardhi yao kwa wafugaji jamii ya wamasai bila ya kuwashirikisha wananchi hali inayotishia kuzuka kwa mgogoro baina ya wafugaji na wakulima.

Kwa upande wao baadhi ya Viongozi wa Kijiji hicho ambao ni Bi Halima Omari na Bwana Paulo Mtinange wamekiri kuwepo kwa mgogoro huo lakini wamekana kuhusika nao kama wanavyodai wananchi.
Kwa mujibu wa wanakijiji hao,mgogoro huo ni wa muda mrefu na kila kiongozi ajaye katika kijiji hicho amekuwa akiuongeza badala ya kuutafutia ufumbuzi kabla haujaleta madhara kama ilivyo kwa maeneo mengine.

No comments:

Post a Comment