KATIBU
Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban Ki
Moon,amesifu jitihada za Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mchango wake
mkubwa katika kupigania Afya ya Mama na Mtoto.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Muandishi wa Habari wa rais msaidizi bwana Premi Kibanga,Bw. Ki Moon ametoa pongezi hizo jana wakati alipokuwa akizungumzia juhudi za kumuokoa Mama na Mtoto ikiwa ni mwishoni mwa mkutano wa siku 3 kuhusu Afya ya Mama na Mtoto uliofanyika nchini Canada.

Rais Kikwete na Waziri Mkuu wa Canada Bw. Stephen Harper, kwa miaka minne wamekuwa Wenyeviti Wenza wa Kamisheni ya Habari na Uwajibikaji katika masuala ya Afya ya Mama na Mtoto , ambayo imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha vifo vya Watoto wachanga na Mama wajawazito vinapunguzwa kwa nusu ifikapo Mwaka 2015.
Pamoja na mafanikio hayo, Rais Kikwete amesema bado jitihada zinahitajika katika kuhakikisha mafanikio hayo yanaimarishwa zaidi na kwamba hayapotei .
Aidha Rais Kikwete amesema Tanzania inahitaji vitega uchumi zaidi kutoka Canada na hivyo kuwakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara wa Canada kuja kuwekeza Tanzania.
Rais Kikwete anatarajia kuondoka Toronto nchini Canada kurejea Dar es Salaam, kupitia Marekani.
No comments:
Post a Comment