Saturday, May 31, 2014

MADIWANI wilayani Kilosa watakiwa kusimamia maendeleo ya taaluma wilayani humo



MKUU wa wilaya kilosa,mkoani Morogoro  Elias Tarimo ametoa wito kwa madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Kilosa  kusimamia maendeleo ya taaluma shuleni kwa kufuatilia utoro wa walimu kama wanaingia madarasani kufundisha na  wanafunzi kama wanahudhuria madarasani .

Wito huo ameutoa hivi karibuni katika kikao cha madiwani kilichofanyika mjini hapo kilichokutanisha madiwani wote wa halmashauri ya wilaya , watendaji kata na wataalamu wa halmashauri ya wilaya
.

Tarimo amesema kuwa wilaya ya kilosa imekuwa na changamoto  ya elimu kutokana na kushuka kwa kiwango cha elimu ambapo mwaka 2013 kiwango kilishuka kutokana na ufaulu wa wanafunzi kufikia asilimia 38 tu.

Ameelza kuwa madiwani wanapaswa kusimamia  utekelezaji wa kiwango cha taaluma shuleni kwani wakati nwingine walimu hawawajibiki ipasavyo kwa kuingia madarasani kwa kufundisha watoto ambapo pia watoto wamekuwa watoro shuleni mitaani kuuza biashara na kuchunga mifugo.

No comments:

Post a Comment