Friday, May 30, 2014

WATU wawili wilayani Kilosa, washikiliwa na polisi kwa tuhuma za wizi wa mifugo



WAKAZI  wawili ambao ni ndugu  jamii ya kimasai Sepuka  Koliji mwenye umri wa miaka (29) na Mogela  Koliji mwenye umri wa miaka (20) wakazi wa kijiji cha parakuyo tarafa ya Kimamba wilayani Kilosa,mkoa wa Morogoro  wanashikiliwa na jeshi la polisi wilayani humu kwa kosa la wizi wa mifugo.

Akizungumza na mbiu ya maendeleo kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paulo amesema kuwa tukio hilo limetokea mapema mwezi huu huko maeneo ya kijiji cha parakuyo wilayani hapa.

Kamanda PAULO amesema kuwa siku ya tukio watuhumiwa hao ambao ni ndugu kwa pamoja waliiba ng’ombe wapatao 21 ambao ni mali  ya ndugu yao ajulikanae kwa jina la Kisonga Koliji ambapo walikutwa wakiwapeleka mnadani maeneo ya melela kwa ajili ya kuwauza

No comments:

Post a Comment