Friday, May 30, 2014

WATENDAJI wa vijiji , wilayani Kilosa wametakiwa kusimamia masuala ya usafi wa mazingira



DIWANI  wa kata ya Masanze wilaya ya  Kilosa,mkoani Morogoro Mheshimiwa Jonathan Kambikiye amewataka watendaji wa vijiji kwenye kata hiyo kusimamia  masuala ya usafi ili kuepuka magonjwa mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa homa ya Dengi  ulioibuka hivi karibuni katika mikoa mbalimbali  nchini.

Akizungumza na Mbiu ya Maendeleo mapema leo mjini Kilosa mheshimiwa Kambikiye amesema, watendaji wa vijiji wanawajibu wa  kuhakikisha kuwa suala  la usafi kwenye kata hiyo linapewa kipaumbele.

Amesema kuwa suala la usafi ni muhimu katika kata hiyo na  wahakikishe wananchimba vyoo , kwa kila kaya sanjari na  kuchimba mashimo ya taka na kufyeka sehemu zenye vichaka.

Mbali na hayo diwani huyo  ametoa wito kwa wataalamu kwenye kata hiyo kutoa ushauri na kushirikiana na watendaji wa kata na vijiji kuhakikisha wanakusanya  mapato  ya vijiji ipasavyo itakayosaidia kuleta maendeleo kwenye kata hiyo.

No comments:

Post a Comment