MAADHIMISHO ya 17 ya wiki ya Maziwa
kitaifa yamezinduliwa leo mkoani Mara ambapo imeelezwa kuwa kiwango
cha unywaji Maziwa bado ni kidogo ikilinganishwa na kile kilichopendekezwa na
Shirika la Chakula na Afya Duniani.
Mwakilishi wa Kaimu Mkuu wa mkoa wa Mara Bw
Jackson Msome ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Musoma ameyasema hayo katika
uzinduzi wa maadhimisho ya 17 ya wiki ya Maziwa katika uwanja wa Shule Msingi
Mukendo Manispaa ya Musoma mkoani Mara.
Amesema lengo la Maadhimisho hayo ni kulenga
shughuli za wadau wa Maziwa ingawa kuna changamoto kubwa kwa viwanda vya
usindikaji Maziwa nchini huku akisema kuwa kutokana na uzalishaji kwa sasa
wastani wa unywaji Maziwa kwa mtu ni lita 45 kwa mwaka huku viwango
vilivyopendekezwa na Shirika la WHO na FAO ni kunywa Maziwa lita 200 kwa
mwaka.
Katika Maadhimisho hayo ambayo kilele chake ni
june mosi mwaka huu shirika la taifa la hifadhi ya Jamii NSSF limeendesha
kambi ya upimaji wa afya bure kwa wakazi wa Mkoa wa Mara ambapo litaendesha
zoezi hilo kwa siku tatu na baadae kuelekea katika mikoa ya shinyanga, Geita na
Kagera
No comments:
Post a Comment