Saturday, December 27, 2014

AZAM FC yaahidi kuwafunga El Merreikh ya Sudan


Wachezaji wa Azam FC wakishangilia ushindi

KLABU  ya Azam ya Tanzania imesema mechi za kirafiki ilizocheza nchini Uganda hivi karibuni zinatosha kuivaa Klabu ya El- Merreikh ya Sudan katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hapo mwakani.

Azam, wakiwa na uzoefu wa miaka miwili katika michuano ya kimataifa na kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara kwa mara ya kwanza tangu ianze kucheza ligi kuu Tanzania bara mwaka 2008, wamepangwa kuwavaa vigogo hao mabingwa mara 19 wa Sudan na wazoefu wa michuano ya kimataifa katika mechi za awali za mtoano zitakazochezwa nyumbani na ugenini.
Msemaji wa Azam, Jafar Idd amesema hawaoni sababu ya kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kujiandaa na mechi hiyo.

No comments:

Post a Comment