Friday, January 22, 2016

RAIS wa China aanza ziara nchini Iran



RAIS  Xi Jinping wa China amewasili mjini Tehran akiongoza ujumbe wa ngazi za juu wa kisiasa na kiuchumi kwa ajili ya kufanya ziara rasmi ya siku mbili  nchini Iran.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari toka nchini Iran , Rais Jinping aliwasili Tehran jana usiku na kupokewa na Muhammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran katika uwanja wa ndege wa Mehrabad.
Miongoni mwa malengo ya ziara hiyo rasmi ya Rais wa China nchini Iran ni kukuza uhusiano wa pande mbili, wa kieneo na kimataifa na vile vile kuongeza ushirikiano katika nyuga tofauti za kisiasa, kiuchumi, kibiashara na kiutamaduni.
Mbali na mazungumzo baina ya marais wawili wa Iran na China na wajumbe wa pande mbili, katika ziara hii Rais Jinping hapa Iran kunatarajiwa kutiwa saini mikataba kadhaa ya ushirikiano katika nyanja za kiuchumi, kisiasa, kisheria na kiutamaduni.
Rais Xin Jinping wa China amekuja nchini  Iran kwa mwaliko wa Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

No comments:

Post a Comment