Friday, January 22, 2016

WANANCHI wakabidhi maiti ofisi ya mkuu wa mkoa


Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk Rajabu Rutengwe

KUNDI la watu zaidi ya wanakijiji 60 wa kijiji cha Mabana wilayani Kilosa wametua ofisini kwa mkuu wa mkoa Morogoro Dk.Rajabu Rutengwe na mwili wa Mkulima Said Madule (76) aliyeuwawa shambani kwake na wafugaji jamii ya Masai ili ashuhudie na kusadiki kuwa kumekuwa kukitokea maafa kila inapotokea msimu wa kilimo mashambani.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti ofisini hapo baadhi ya wanakijiji hao na wanafamilia walisema wameamua kufanya hivyo ili kumsadikisha mkuu wa mkoa huo,mkuu wa polisi na usalama kuwa jamii hiyo inanguvu ya kufabnya lolote kwa wakulima bila serikali kuchukua hatua zozote za kisheria.

"tumelia sana,tumesema sana lakini hayo yote yamepuuzwa na viongozi wote kuanzia wa vyama vya siasa ngazi zote hadi wa serikali ngazi zote hapa mkoani...hasa jeshi la polisi wilayani kwetu tunadiriki kusema limemezwa na wafugaji kwa asilimia zote" alisema Masudi Mohamedi (76)

Wakionyesha kuchoshwa na utendaji wa jeshi hilo kuanzia kituo kidogo kilichopo Dumila hadi wilaya hiyo ya Kilosa walisema tarehe 17. Januari  Marehemu Mzee Said alikwenda shambabni kwake kutazama mazao yake ya Tikiti ambapo alikuta kundi la Ng'ombe waliotajwa kuwa mali ya mfugaji aliyetambulika kwa jina la Leteo.

Walisema alipojaribu kuwaondoa shambani humo,ghafula alivamiwa na wafugaji hao kisha kumjeruhi kichwani karibu na kosogo na sime kisha kutoweka baada ya mzee huyo kupoteza fahamu na kuanguka chini ambapo aliokotwa na shemeji yake Tabu Ambuje(65).


Katika tukio hilo wanakijiji walifanikiwa kukamata kundi la Ng'ombe waliokuwa shambani humo kisha kuwahifazi ofisi ya mtendaji kijiji sambamba na mmilikiwake aliyetajwa kwa jina la Leteo aliyefikishwa polisi kituo cha Dumila ili ashikiliwe hadi hali ya mgonjwa itakapokuwa nzuri

Tofauti na walivyodhani na kuelewa mfugaji huyo aliachiwa siku hiyo hiyo na kuja kuchukua Ng'ombe hao kwa kulipa kwa mtendaji wa kijiji hicho cha Mabana faini ya shilingi 150,000, walipouliza kituoni kulikoni aachiwe mtuhumiwa aachiwe ilihali mgonjwa hali yake ni mbaya walijibiwa wajali kuuguza mambo ya polisi hayawahusu.

Mbali na majibu hayo kituo kidogo cha polisi Dumila,pia walipojarubu kupata ufafanuzi juu ya taratibu za dhamana kwa mtuhumiwa aliyejeruhi polisili wilayani Kilosa,walijibiwa kuwa jukumu lao ni kuzika kama hawataki wakae na maiti hadi atoe harufu ndio wazike.

Hata hivyo juhudi za kuonana na mkuu wa mkoa huyo zilishindikana na kushauriwa na badhi ya walinzi ofisini hapo kwenda kwa kamanda wa polisi mkoa kwakuwa ni mkuu wa ulinzi na usalama mkoani humo.

Kufuatia mjadala huo wa mda mrefu kamanda wa polisi mkoani Morogoro Leonard Paul alikwenda kijijini Mabana na kuwaeleza wananchi msibani kuwa jeshi linakili kuwepo uzembe katika utendaji nakuwa mara moja litachukua hatua kali dhiidi ya wahusika wote juu ya afa hilo na mengine yatakayotokea.

No comments:

Post a Comment