Thursday, November 10, 2016

OBAMA aahidi kumuunga mkono Trump

Rais mteule wa Marekani Trump (kushoto) na Rais wa  Obama (kulia)
RAIS mteule wa Marekani Donald Trump amesema kuwa ni ''heshima'' kubwa kukutana na rais Barrack Obama katika mazungumzo ya mpito yaliofanyika katika ikulu ya White House.

Bwana Obama amesema kuwa ametiwa moyo kuhusu mazungumzo yao ya maswala mbalimbali yaliochukua zaidi ya saa moja.
Bwana Trump ametilia shaka uraia wa rais Obama na kuapa kuharibu ufanisi wake wakati wa utawala wake.
Wakati wa kampeni bwana Obama alisema kuwa bwana Trump 'hafai' kuongoza Marekani.
Hata hivyo Obama alisema kuwa ''anamuunga'' mkono baada ya kumshinda Hillary Clinton.


No comments:

Post a Comment