BAADA ya wananchi kuchoshwa na
kukamatwa mikutanoni na kuswekwa lumande kwa kuhoji mapatao na matumizi baadhi
yao wameibuka na kuliangukia shirika Foundation for civil society-FCS na
washirika wake kupatia elimu ya uraia ili wapate misingi na nguvu ya kuhoji
matumizi mabaya ya rasilimali zao za umma vijijini.
Hayo yameibuka kwenye mafunzo ya
utawala bora sambamba na ufuatiliaji rasilamali za umma sekta ya elimu tarafani
humo yaliyotolewa na asasi ya Chayode ikishirikiana na FCS kwa viongozi wa
serikali, walemavu,wananchi,waratibu elimu na walimu, kutoka kata ya Mgeta na
Bunduki tarafani humo katika sekondari Mgeta.
Mjumbe wa bodi ya sekondari Bunduki…
akisimulia alivyokamatwa kwa kuhoji sababu za kutosomewa taarifa ya mapato na
matumizi alisema viongozi wa serikali ni miungu watu na ‘wapigaji dili’ wakubwa
wa rasilimali za umma kutokana na kinga waliyoanyo ya kumweka ndani mtu yeyote
kama alivyofanyiwa yeye 4.Februari 2016.
“4.Februari 2016 kulikuwa na mkutano
kijijini Maguruwe katika mkutano ule mbali na mambo mengine mimi nilimuuliza
mwenyekiti zilipo shilingi Mil 2 tulizokuwa tumepewa na mfadhili kujengea
vyumba viwili vya madarasa sekondari yetu ya Bunduki…kilichofuata ni agizo la
mimi kukamatwa na kuwekwa ndani kwa kuharibu mkutano”alisema…
Aliongeza kuwa ndioa maana mikutano
ya vijiji haiitishwi na hakuna hata kiongozi wa kulisimamia hilo badala yake
wanachi tukihoji wanawekwa ndani kwa muda usiojulikana ili kuwatisha na kuwazib
No comments:
Post a Comment