LAANA na maagizo mazito kwa vyombo vya dola dhidi wazazi na walezi wa
Mtoto marehemu Nasra Rashidi(4) yametolewa leo na viongozi wa
serikali na dini Mkoani Morogoro wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa
mtoto huyo uwanja wa Jamuhuri.
Katika salamu za mkoa kwa mamia ya
watu uwanjani hapo mbele ya jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu Nasra,Mkuu
wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera aliiomba Mahakama na jeshi la polisi mkoani
humo kutokuwa na huruma na wazazi hao.
"bila kutafuna maneno,huruma
wala haya kwa yeyote hapa ukatili huu uliomfungulia pepo mtoto huyu baada ya
kufanyiwa ukatili,fedheha kwa mkoa na Taifa dhambi hii iwatafune kuanzia sasa
hapa hapa duniani na hata baadae mbinguni"alisema Bendera akionyesha
kububjikwa machozi.
Katika salamu hizo mkuu huyo alisema
haiingii akilini kwa mtoto mwenye baba,mama ndugu na jamaa wachamungu kupitia
dini fulani duniani akafichwa na kuteswa kwenye boksi kwa zaidi ya miaka mitatu
kwa sababu ya aina yoyote iliyopo hapa duniani halafu akafurahiwa.
"jamani tumuogope mungu na
kumtii Mungu, haifurahishi wala haifai hata kusimulia nawaomba Mahakama
mkishirikiana na polisi upelelezi hawa ambao hata dhamana wamekosa wateseke
kama alivyo teseka mtoto Nasra"aliongeza
Kwa upande wa mbunge wa jimbo la
Morogoro Abdulahzizi Abood alisema msiba wa Nasra umekuwa gumzo
katika vikao vya Bunge vinavyoendelea mjini Dodoma na kuamsha fedheha nyingine
kwa taifa ukiuonyesha mkoa kutokuwa na huruma ya ukatili kwa watoto.
"kama kuna wengine wanafanya
hivi binafsi nawasihi waache na kama hawawataki watoto hao wawalete tuwatafutie
watu wa kuwale,nin aimani wapo wanatafuta watoto"alifafanua Abood.
Akihitimisha maombolezo uwanjani
hapo Shekhe wa Morogoro Ally Omari alisema mateso ya mtoto huyo hayawezi
kutenganishwa na ushirikina kwakuwa wazazi na walezi walilifahamu jabo hilo na
kuendelea na shuguli zao ikiwemo sokoni na mama lishe.
Akionyesha kukerwa na mtoto huyo
kufanywa 'Ndondocha' Shekhe Omari alisema wazazi wa sasa wakiwemo wa
Marehemu Nasra wanalaa zinaa 'Michepuko' ambayo mwisho wake ni aibu kama
iliyojitokeza katika msiba huo.
No comments:
Post a Comment