Tuesday, June 3, 2014

WAKULIMA wa kilimo cha umwagiliaji waiomba serikali kuwapatia wataalamu wa mazingira ili kukabiliana na changamoto


WAKATI tukielekea kuadhimisha siku ya mazingira duniani ambayo  hufanyika juni 5, kila mwaka wakulima wa kilimo cha umwagiliaji Msosa wilayani Kilolo mkoani Iringa wameiomba ofisi ya makamu wa Raisi kitengo cha mazingira kuongeza kasi ya utoaji wa elimu ya uhifadhi wa mazingira  kwa wakulima wadogo wadogo
.

Wakiongea na mbiu ya maendeleo mapema jana katika vijiji vya Mtandika na Msosa wilayani humo . wakulima hao wamesema  kuwa mabadiliko ya tabia nchi yanakuja kwa kasi sana na ndio maana kuna mambo yanatokea kila uchao na uchwao hivyo ni vyema wakulima wakaelimishwa  mbinu mbadala ya kukabiliana na hali hiyo.
Wamesema wao, wanatumia mbolea za viwandani katika kuzalisha mazao mbalimbali ukizingatia tunatumia kilimo cha umwagiliaji ambacho kina hitaji wataalamu wa masuala ya mazingira kabla ya utekelezaji wake, lakini kutokana namchakmchaka wa mapambano ya umaskini kupitia sekta hiyo sanjari na uhaba wa wataalamu wa mazingira ngazi ya wilaya, sehemu kubwa  tunalima kienyeji zaidi.

Siku ya mazingira kitaifa mwaka huu inafanyika mkoani Mwanza  ikiwa inapambwa kwa shughuli mbalimbali za usafi wa mazingira ikiwa na kauli mbiu “Tunza mazingira kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi”


Bwawa la Mtera lililopo kijiji cha  Mkungugu, tarafa ya Ismani ,mkoani  Iringa ambalo hutumiwa kwa kilimo cha umwagiliaji katika vijiji vinavyozunguka bwawa hilo

No comments:

Post a Comment