UHABA wa vifaa vya kisasa na wataalamu wa mazingira ni miongoni mwa ni mambo yanayochangia kukithiri kwa uchafu katika masoko mengi jijini Dar es
salaam. IMEELEZWA
Wafanyabiashara wa nazi katika soko
la Ilala, jijini Dar es salaam wameeleza
hayo leo katika mahojiano maalum
na mbiu ya maendeleo.
Wamesema wafanyabiashara wengi
wanalipa ushuru wa soko kama unavyohitajika lakini mara nyingi majiibu ya
uongozi ni kukosekana kwa wataalamu wa
kutosha wa masuala ya mazingira katika soko hilo sanjari na uhaba wa vifaa.
Hata hivyo wametaka mamlaka husika
kutafuta mzizi wa matatizo hayo kwani hali ya soko hiklo kiafya ni mbaya sana
kutokana na bidhaa nyingi kupangwa chini hali inayotishia usalama wa mlaji kiafya.
No comments:
Post a Comment