Wednesday, June 4, 2014

WANAKIJIJI wavamia shamba la mwekezaji kinyemela


WANAKIJIJI wa kijiji cha Lubungo A kata ya Mikese wilayani Morogoro wamevamia shamba linalodaiwa kupewa mwekezaji kinyemela na uongozi wa kijiji wakishirik shamba la mwekezaji kinyemela i na wilaya na kugawiana kisha kukesha wakifyeka msitu kwa walichodai wamechoshwa na maamuzi yasiyowashirikisha ya kidikiteta.


Uvamizi huo unaohusisha eneo hilo linalokadiriwa kuwa na ukubwa wa ekari 1000 unatokana na wanakijiji hao kubaini kuwa eneo hilo ambalo hawajawahi kulipangia matumizi linakodishwa kwa watu baki na kufyekwa msitu uliokuwepo kwa maandalizi ya mashamba.

Wakizungumza kwa nyakati toafuti mashambani wakisafisha mashamba wanakijiji Shabani Salumu(38) Ester Daud(45)na Huseni Mzuri(43) walisema wamechoshwa na rushwa kwa viongozi wao na kuuza eneo lote kwa wawekezaji bila hata taarifa.

Wanakijiji hao walisema wameamua kupiga kambi kijijini hapo wakilenga kutanua uzalishaji la kutimisha ndoto ya rais Jakaya Kikwete aliyoitangaza kwenye uwanja wa Jamuhuri mjini Morogoro kuwa mkoa wao umeteuliwa kuwa ghala la taifa la chakula na kufikia sera ya matokeo makubwa sasa.
Alipotafutwa kutoa ufafanuzi wa tatizo hilo Mwenyekiti wa kijiji hicho Juma Mgunda mbali na kukili kuwepo ongezerko la wananchi kijijini hapo na eneo kupungua 
Hata hivyo alisema zaidi ni elimu ya sheria zinazotawala masuala ya ardhi ikilinganishwa na mabadiriko ya sheria hizo hasa kwenye sheria ya ardhi ya mwaka 1999 iliyobadilisha mfumo wa matumizi na utoji ardhi kwa wanakijiji na wawekezaji katika jamii.


No comments:

Post a Comment