KESHO ni maadhimisho ya siku ya mazingira duniani ambapo kitaifa
yatafanyika jijini Mwanza ambapo kutapambwa na shughuli mbalimbali za usafi wa
mazingira ikiwemo kusafisha maeneo , kuzoa taka,kupanda miti inayofaa n.k
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa hivi
karibuni na waziri ofisi ya makamu wa Raisi
(mazingira) Dk Binilith S. Mahenge kwa vyombo vya habari nchini, watanzania
tutaungana na mataifa mengine kuadhimisha siku ya mazingira duniani ambayo
hufanyika juni 5, kila mwaka .
Waziri Mahenge
wamewataka watanzania kutunza mazingira na kutoachoma moto hovyo ili kukabiliana na
mabadiliko ya tabia nchi ambayo ynakuja
kwa kasi kubwa nchini na duniani kwa ujumla .
Kwa mujibu wa taarifa ya
tano ya jopo la wataalamu wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, sekta
ya nishati inachangia asilimia 25,sekta ya kilimo, misitu na matumizi ya ardhi
inachangia asilimia 24,viwanda 21 usafirishaji asilimia 14
na sekta nyingine asilimia 9.6 shughuli hizi ndizo chanzo cha ongezeko la
gesijoto duniani.
No comments:
Post a Comment