Tuesday, July 15, 2014

KANISA la Anglikana laidhinisha wanawake kuwa maaskofu



The General Synod katika kikao cha mjadala
BARAZA  kuu la kanisa la Kianglikana Uingereza, The General Synod, limeidhinisha wanawake kuwa maaskofu.

Maafisa katika kanisa hilo wanaamini wana ufuasi mkubwa unaounga mkono hoja hiyo.
Sasa baada ya kupitishwa kwa kura hiyo, huenda askofu wa kwanza mwanamke akachaguliwa kufikia mwishoni mwa mwaka huu.
Makasisi wanawake walio thuluthi moja ya viongozi wa kidini wa kanisa la kianglikana, wanasema haki sawa itawapandisha hadhi katika makanisa.
Hatua hiyo inamaliza mvutano wa miaka mingi na kuvunja utamaduni wa makarne katika kanisa hilo. Tofauti nyingi zimeibuka kuhusu suala hilo na hata kusababisha migawanyiko katika kanisa hilo ambapo baadhi ya ma dayosisi yameshawatawaza maaskofu wanawake, na kukaidi amri la hapo awali la kanisa kuu.
Nchi zilizo na maaskofu wanawake:New Zealand,Australia,Marekani,Canada na Afrika Kusini

No comments:

Post a Comment