Amir wa Qatara Tamim bin Hamad Aaal Thani |
AMIR wa Qatar amemtaka Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban
Ki moon achukue hatua za maana ili kukomesha jinai za utawala wa Kizayuni wa
Israel dhidi ya wananchi wa Ghaza huko Palestina.
Tamim bin Hamad Aal Thani ametoa takwa hilo
katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na Ban Ki-Moon na kusisitiza kwamba,
jamii ya kimataifa na Baraza la Usalama linapaswa kutekeleza majukumu yake
ipasavyo ambapo mbali na kukomesha jinai za Israel ziwaunge mkono wananchi
madhulumu wa Palestina.
Aidha Amir wa Qatar amefanya
mazungumzo kwa njia ya simu na Recep Tayyib Erdogan Waziri Mkuu wa Uturuki na
kujadiliana naye udharura wa kuweko juhudi za pamoja za kuwasaidia wananchi wa
Palestina.
Wakati huo huo, jinai za Israel huko Ghaza
zimeendelea kulaainiwa katika kila pembe ya dunia na kutolewa miito ya
kukomeshwa jinai hizo. Chama tawala cha African National Congress nchini Afrika
Kusini kimetangaza kwamba, utawala wa Kizayuni wa Israel unapaswa kusimamisha
haraka iwezekanavyo mashambulizi yake ya kijeshi na kuondoa mzingiro wa
kidhulma dhidi ya wananchi wa Palestina walioko katika eneo la Ukanda wa Ghaza.
Tanzania pia imetaka kukomeshwa mara moja
mauaji huko Ghaza.
No comments:
Post a Comment