Thursday, July 3, 2014

WANANCHI jijini London, Uingereza waandamana kuikosoa BBC


Waandamanaji jijini London ,nchini Uingereza
WANAHARAKATI  na wananchi wa jiji la London, Uingereza jana waliandamana mkabala wa ofisi kuu ya Shirika la Habari la Uingereza BBC wakikosoa vikali jinsi lilivyokuwa likitangaza habari zinazohusiana na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi wa Palestina.

Waandamanaji hao wamelilalamikia shirika la BBC katika kuainisi habari zinazohusiana na Palestina. Wananchi na wanaharakati hao wameeleza kuwa, katika siku za hivi karibuni shirika hilo limekuwa likitangaza mara kwa mara habari zinazohusiana na kupatikana viwiliwili vya Wazayuni watatu; lakini limenyamazia kimya kutangaza habari ya kuuawa shahidi siku hiyohiyo kijana wa Kipalestina.
Hali kadhalika, shirika la BBC linatuhumiwa kwa kutoeleza wazi kwamba mji wa Baitul Muqaddas, kuwa ni mji unaokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel. Waandamanaji hao walikuwa wamebeba mabango na maberamu yaliyoandikwa kuwa, 'Msizichuje habari za Palestina'.






No comments:

Post a Comment