Thursday, July 3, 2014

SUDAN kusini huenda ikakumbwa na upungufu wa chakula mwezi ujao


Wananchi wa Sudan kusini
TAKRIBAN watu milioni nne nchini Sudani kusini wako hatarini kukabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula mwezi ujao, Mashirika ya misaada ya Uingereza yametaadharisha.

Zaidi ya Watu milioni moja wamekimbia makazi yao baada ya kuibuka mapigano mwezi Desemba mwaka jana kati ya makundi yanayokinzana ya Chama kinachotawala nchini humo.
Maelfu ya watu wamepoteza maisha kutokana na mgogoro ulioanza kama mgogoro wa kisiasa kati ya Rais wa Sudani kusini, Salva Kiir na aliyekua makamu wake,Riek Machar.
Kamati inayoshughulikia majanga ambayo inashirikiana na mashirika 13 ya misaada kutoka Uingereza ambayo hushughulikia majanga kimataifa,imesema

No comments:

Post a Comment