Vijana waliotahiriwa nchini Afrika kusini |
WIZARA ya Afya
nchini Afrika Kusini inasema kuwa wavulana kumi na tisa wameaga dunia mwaka huu
katika sherehe za kitamaduni za kuwapasha tohara wavulana.
Utamaduni wa tohara ni muhimu kwa
vijana hasa kwa kuwa ni njia ya vijana kuingia utu uzima, lakini baadhi
hufariki wakipitia utamaduni huo na wengine hupoteza sehemu zao nyeti.
Vijana 19 wamefariki kufika sasa na
wengine 50 wako hospitalini wanapokea matibabu ya kukosa maji mwilini, sehemu
zao za siri kuoza na majerahe mengine mabaya.
Wazee wa kijamii wasiokuwa na
mafunzo ya kufanya tohara ambao huendesha vituo vya kuwapasha tohara vijana
wamelaumiwa kwa vifo kama hivyo.
No comments:
Post a Comment