Skauti wakiwa mazoezini |
SERIKALI imeombwa kutenga bajeti maalumu itakayotolewa ruzuku
kwa vijana SKAUTI nchini ikwa ni hatua mojawapo ya kuwaandaa vijana nchini
kuwa na uzalendo.
Ombi hilo lilitolewa na Kamishina
Mkuu Msaidizi program za vijana(SKAUTI )Mary Anyitike kwenye hafla fupi ya
kutoa nishani kwa viongozi wa SKAUTI kituo cha BAHATI CAMP Morogoro na kufunga
mafunzo ya skauti kutoka mkoani Dar es salaam,Morogoro, Shinyanga ,Pwani
na Mbeya.
Katika hafla hiyo Kamishina huyo alisema mbali na vijana
kijitokeza kwa kiwango kidogo kushiriki katika mafunzo na shuguli za maendeleo
bado kunachangamoto ya kutokuwa na fungu uendeshaji hasa katika kugharimia
shuguli walizonazo.
Aidha aliongeza kuwa skauti Tanzania wanakabiliwa na
changamoto mbalimbali ikiwemo vijana kujigharimia wenyewe,kushindwa
kujipima kama program zao zinaendana na zile za nje na vijana kushindwa
kushiriki mafunzo.
Kwa upande wake Mtahini Mkuu katika
Kambi ya Skauti Mkoa wa Morogoro ( BAHATI CAMP) John Lusunike alisema bado
taaluma ya skauti iko chini huku akiwataka viongozi na wawakilishi kuhakikisha
wanalipa kipaumbele suala hilo.
No comments:
Post a Comment