SHeikh mkuu wa Dar es salaam Alhad Musa Salum |
SHEIK Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam nchini Tanzania amewataka Waislamu kunufaika vyema na ibada tukufu ya Hija.
Sheikh al-Hadi Mussa Salum amesema hayo katika mahojiano maalumu na wanahabari.Amesema kuwa, Hija ni mkusanyiko mkubwa zaidi wa Waislamu hivyo wafuasi wa dini hii wanapaswa kuitumia ibada hii kwa ajili ya kudumisha umoja na mshikamano baina yao.
Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam amewataka mahujaji mbali na kunufaika vyema na masuala ya kimaanawi, kuhakikisha pia wanafaidika na manufaa mengine ya kiuchumi na kijamii yanayopatikana katika ibada hiyo tukufu. Sheikh al-Hadi Mussa Salum amekemea vikali vitendo vya jinai na mauaji ya makundi ya kigaidi yanayofanya mauaji ya kinyama kwa jina la Uislamu na kubainisha kwamba, Waislamu wanapaswa kufanya kila wawezalo kuutambulisha Uislamu sahihi mbele ya walimwengu.
No comments:
Post a Comment