Tuesday, September 23, 2014

QATAR matatani kuhusu kombe la dunia 2022


Aliyekuwa katibu mkuu wa FIFA Hammamu
RIPOTI iliyotolewa kuhusu tenda ya kuhodhi michuano ya kombe la dunia kwa mwaka 2018 na mwaka 2022 imeelezwa huenda ikasabisha wanaoshutumiwa kufunguliwa mashtaka.

Mbunge wa chama cha Conservative nchini uingereza, Damian Collins aliitaka ofisi inayochunguza maswala ya udanganyifu na rushwa kuomba nakala ya ripoti iliyotolewa kuhusu mchakato wa kutoa tenda kwa ajili ya michuano ya kombe la dunia mwaka 2018 na 2022, akisema kuwa anaamini Ripoti hiyo huenda inatoa ushahidi kuhusu madai ya vitendo vya rushwa.
Mwanasheria kutoka nchini Marekani, Michael Garcia alitoa ripoti yake mwezi huu, lakini Fifa imesema yaliyomo kwenye ripoti hiyo hayatatolewa hadharani


No comments:

Post a Comment