MAKUNDI
maalumu katika jamii likiwemo la
walemavu,vijana na wanawake mkoani Morogoro wametabiri machafuko ya kisiasa
nchini katika chaguzi zijazo za serikali kutokana na serikali kufumbia macho
rushwa na kuwaogopa mabepari wenye fedha katika harakati za uchaguzi.
Hayo yamebainishwa kwa nyakati
tofauti mjini hapa na mwenyekiti wa wenye Ualubino mkoani Morogoro David
Mganga,mjasiliamali wilayani Mvomero Joyce White na Mwenyekiti wa chama cha
Jahazi asilia Ismail Ismail mara baada kukutanishwa.
Walisema hofi ya kuhujumiwa na
wenyefedha kwa uchaguzi unaotaraji kuanza na serikalia za mitaa mwezi
Desemba na kukamilishwa mwakani na serikali kuu haitokanani tu na nguvu
ya fedha bali inatokana na jinsi serikali inavyo waogopa matajiri.
Hata hivyo walitaja changamoto
zinazowakabili kutojitokeza kuwania uongozi mbalimbali kuwa ni pamoja na
kuendelea kwa mifumo Dume katika jamii,umasikini,ubaguzi wa jinsi na hofu ya
kuuwawa hususani kwa wenye ulemavu wa ngozi.
Mratibu wa mafunzo hayo
yaliyoandaliwa mtandao wa jinsia nchini TGNP na kituo cha haki za binadamu
LHRC, Happy Maruchu alisema lengo la kuwakutanisha ni kuwajengea uwezo
makundi hayo kuingia na kuwania nafasi mbalimbali za uongozi.
Uchaguzi wa serikali za mitaa nchini
unataraji kufanyika nchini kote mwezi Desemba licha ya mvutano mkubwa baina ya
wadau wa uchaguzi vikiwemo vyama vya siasa,asasi za kiraia,makundi maalumu nan
tume ya uchaguzi kuvutana na serikali juu ya lini ufanyike.
No comments:
Post a Comment