Tuesday, September 23, 2014

KVTC yagawa pikipiki 23 kwa wafanyakazi wake


KAMPUNI ya Mitiki bonde la mto Kilombero iliyopo wilayani Kilombero imemwaga pikipiki 23 zenye thamani ya shilingi Mil.70 kwa wanachama wa SACCOS ya wafanyakazi wa kampuni hiyo 'KVTC Workers Saccos' wilayani humo.


Katibu wa KVTCWorkers Saccos Kennedy Haule alisema pikipiki hizo zitakazokopeshwa kwa bei nafuu wanachama wa saccos hiyo zimetolewa sambamba na kuwapunguzia tatizo la usafiri pia kuwapunguzia umasikini kwa kujikusanyia fedha kwa kusafirisha abilia. 


Alisema pikipiki hizo zenye uwezo wa kubeba mzigo wa hadi tani mbili zinazokusudiwa kupunguza muda,gharama zqa uzalishaji na kubebea mizigo toka mashambani zinatakiwa kuwa zimelipwa deni lake ndani ya mwaka mmoja ili wanachama wengine wakopeshwe haraka na kujikwamua kiuchumi.

Hata hivyo Haule alibainisha mafanikio yaliyofikiwa kuwa ni upatikanaji wa Power tiller Nane za shilingi Mil.52 mwaka 2008,mashine zenye uwezo wa kutoto mayai 60 kwa mkupuo na kununua mashine ya kutengenezea mkaa kupitia mabaki ya mbao viwandani.

Baadhi ya wanachama akiwemo Irine Mathew na Ally Maganga walisema kuwa saccos hiyo ni mkombozi katika maisha yao kutokana na kuwaongezea kipato marambili zaidi ya walichokipata awali hivyo kuwawezesha kumudu gharama za maisha.
Saccos ya KVTC ilianzishwa mwaka 2011 na kusajiliwa mwaka 2014,ina wanachama 75 wakiwemo wafanyakazi na wastaafu wa kampuni hiyo iliyoanza na mtaji wa shilingi laki 5 na sasa myaji wake ni shilingi mil 200 ikiwa na miradi mbalimbali ukiwemo wa kilimo cha mitiki na kukopeshana katika mfumo wa fedha na vifaa.




No comments:

Post a Comment