Friday, September 19, 2014

UJENZI wa bwawa la An NAHDHA si tishio kwa Misri




Bwawa la An Nahdha
HAILEMARIA Desalegn Waziri Mkuu wa Ethiopia amesema kuwa, ujenzi wa bwawa la an Nahdha pambizoni mwa Mto Nile hautakuwa tishio kwa Misri wala nchi yoyote nyingine ya Kiafrika.

Akizungumza na ujumbe wa Bunge la Sudan mjini Addis Ababa, Desalegn ameongeza kuwa, shabaha kuu ya Ethiopia ya kujenga bwawa hilo ni kuzalisha umeme kwa matumizi ya ndani na nchi jirani na kusisitiza kwamba, mpango huo hautaleta madhara na hasara kwa Misri na wala Sudan.
Hatua ya Ethiopia ya kupindisha mkondo wa maji ya Mto Nile kwa shabaha ya kujenga bwawa la kuzalisha umeme, imelalamikiwa vikali na Misri ambayo inadai kwamba ujenzi huo utapelekea kupungua hisa ya maji ya Misri na kusababisha hasara kubwa katika sekta ya kilimo nchini humo.


No comments:

Post a Comment