Jengo la manispaa ya Morogoro |
BAADA ya vyombo vya dola kushindwa
kabisa kumnasa mafichoni mwizi wa vitabu vya kukusanyia maduhuli ya serikali
aliyekuwa mtendaji kata ya Mkuyuni Amosi Mbugulu, Halmashauri ya wilaya ya
Morogoro imewaangukia wanachi nchini ikiwaomba kumfichua aliko ili akamatwe
kuikabili kesi yake Na MOR/RB/8013/2014.
Kwa mujibu
wa mkurugenzi wa halmashauri hiyo Yona Maki kwenye baraza la madiwani ,Mbugulu
alitoweka na vitabu hivyo vya ushuru wa soko tangu mwezi Julai na amekuwa
akitafutwa bila mafanikio.
Vitabu
anavyodaiwa kutoweka navyo ni pamoja na chenya namba 131701-131800 chenye tozo
la sh.400, 192901-193000 tozo la sh.200, 195201-1953300 cha tozo la
sh.200, 198001-198100 cha tozo la sh.200 na 198101-198200 cha tozo la sh.200.
Alisema
juhudi za kumpata zimegonga mwamba kutokana na taarifa za kazi za mtendaji huyo
kutokuwa sawa kutokana na kuhamishwa hamishwa kutoka kata moja kwenda nyingine.
Mkurugenzi
huyo alilazimika kuwaangukia wanachi nchini kote baada ya diwani wa kata ya
Kiroka Robert Selasela aliyetaka kujua kwanini mtendaji huyo hajakamatwa mpka
sasa na ni hatua gani zimechukuliwa dhiidi yake.
“Mwenyekiti
tungependa kujua mkurugezi amechukua hatua gani dhiidi ya mtendaji huyo na kwa
nini hajakamatwa mpka leo… kesi yake imefikia wapi? Amesimamishwa! Au amehamishiwa
wapi na kwa nini?”Alihoji Selasela
No comments:
Post a Comment