Ehud Barak |
Ehud Barak Waziri Mkuu wa
zamani wa utawala wa Kizayuni wa Israel amesema kuwa, utawala huo hauna uwezo
wala nguvu za kupambana kijeshi na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Kwenye
mahojiano aliyofanyiwa na gazeti la Haaretz linalochapishwa huko Israel, Ehud
Barak amesisitiza kwamba, wakati Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa Israel
akihubiri na kutoa kauli za vitisho vya kutaka kuishambulia kijeshi Iran,
anapaswa kwanza kufikiria mpango wa kutatua matatizo ya kiuchumi yanayoukabili
utawala huo. Ehud Barak ameongeza kuwa, wakati alipokuwa Waziri Mkuu wa Israel,
jeshi la utawala huo lilipinga vikali mpango wowote wa kutaka kuishambulia
kijeshi Iran, kutokana na hofu ya radiamali ya kijeshi itakayoonyeshwa na
serikali ya Tehran na jamii ya kimataifa. Barak ambaye aliwahi pia kuwa Waziri
wa Vita wa Israel amebainisha kuwa, kuna umuhimu wa kutatuliwa mushkeli ulioko
kati ya utawala huo na Wapalestina.
Ehud Barak
amehoji kwamba, wakati utawala ulioko madarakani unashindwa kupambana na
wanamgambo wa Hamas, vipi utaweza kutumbukia kwenye vita dhidi ya taifa lenye
nguvu kama Iran? Kwenye mahojiano hayo, Waziri Mkuu wa zamani wa Israel
ameufananisha utawala wa Israel na utawala uliopita wa kibaguzi huko Afrika
Kusini. Inafaa kuashiria hapa kuwa, Ehud Barak aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa
Israel kuanzia mwaka 1999 hadi 2001 na
No comments:
Post a Comment